Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, April 25, 2017

DC MBEYA AWATOROKA WAKUU WA IDARA AKAGUA USAFIMkuu wa wilaya ya Mbeya William Ntinika, jana ameonekana katikakati ya Jiji la Mbeya akikagua usafi wa mazingira peke yake huku akipokea simu na kuwaambia kuwa yupo site.

Katika ziara yake hiyo ya kushitukiza ameifanya leo akianzia katika eneo la Mbeya Retco zilizopo Stationery, wauza magazeti na mafundi viatu.

Akizungumza na mtu mmoja mmoja katika maeneo hayo, aliwaelekeza umuhimu wa kutunza mazingira na kufanya usafi hali inayoweza kuvutia zaidi wateja na wao wenyewe kuwa na amani.

Mmoja wa fundi viatu wa eneo hilo Robert Mwakisyala amesema amefurashwa na utaratibu wa Mkuu huyo wa wilaya wa kuwatembelea kila mmoja mmoja badala ya kuwakusanya.

"Huyu Mkuu wa wilaya ana hekima sana. Ametuelekeza namna tunavyoweza kutunza mazingira yaliyopo mbele yetu ikiwa ni pamoja na kufyeka nyasi kwenye viunga" alisema Mwakisyala.

Akizungumza na baadhi ya watumishi ambao aliwakuta katika eneo la mafundi viatu alisema ameona ni jambo jema kufanya ziara akiwa peke yake na kuzungumza na wafanyabiashara na wananchi wa kawaida mitaani badala ya kusubiri kero ofisini.

Muuza Magazeti katika eneo hilo Zephania Rauta alisifu utaratibu wa kiongozi huyo na kwamba ziara za kushtukiza atajionea uhalisia na kusikia mambo mengi tofauti na angeambatana na watumishi wa idara husika.

"Utaratibu huu auendeleze na akimaliza ziara yake aende akawaulize watumishi aone uhalisia kati ya aliyoyaona na kutushauri na atakayoambiwa" alisema Rauta.

No comments: