Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Monday, April 24, 2017

IFISI HOSPITALI YAWAKUMBUKA WENYE UALBINO MBEYA

Viongozi wa Hospitali teule ya wilaya ya Mbeya Mbalizi Ifisi (wa kwanza kushoto na wa pili), inayomilikiwa na kanisa la Uinjilisti Tanzania, wakiwa na viongozi wa chama cha wenye ualbino Mkoa wa Mbeya na Songwebaada ya kuwakabidhi vifaa vya kujikinga na mionzi ya jua pamoja na mafuta ya kupakaa.

 Na GORDON KALULUNGA, MBEYA

Hospitali teule ya wilaya ya Mbeya Mbalizi Ifisi, imewapatia vifaa vya
kujikinga na mionzi ya jua inayosababisha kansa mwililini kwa watu
wenye ualbino wanaoishi wilayani humo.

 
Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa watu hao mwishoni mwa wiki katika hospitali hiyo.

 
Akikabidhi vifaa hivyo, Katibu wa Hospitali hiyo Emmanuel Martin
alisema hospitali hiyo kwa kufuata mwongozo wa serikali inatoa huduma kwa makundi maalumu ikiwemo watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino.

 
"Kupitia mfuKo wa afya wa pamoja ( Basket Fund) na wahisani wengine Hospitali ina utaratibu wa kutoa Kofia, Miwani na mafuta ya kuzuia mionzi hatari kwa ngozi ambayo inaweza sababisha cancer ya ngozi kwa watu wenye ualbino)"

 
"Bado vifaa vinapatikana na Hospitali inaendelea kutoa vifaa hivyo kwa wahusika pindi wafikapo  hospitali" alisema Katibu huyo.

 
Mwenyekiti wa chama cha wenye Ualbino mkoa wa Mbeya Claud Mwakyoma aliushukuru uongozi wa hospitali hiyo na kwamba changamoto inayowakabili ni walengwa wengine kushindwa uwezo wa kusafiri na kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kupatiwa vifaa hivyo.

 
"Kutokana na changamoto hiyo ndiyo maana tumeweza kufika hapa watu 9 kati ya 68 tunaoishi katika wilaya hii wenye mahitaji na inasikitisha kuona upotoshaji wa baadhi ya viongozi wa Halmashauri kwamba uongozi wa Hospitali hii unakataa kutupatia vifaa" alisema Mwakyoma.

 
Kwa upande wake Katibu wa chama hicho mkoa wa Mbeya na Songwe William Sisala Simwali alisema wilaya zingine zinapaswa kuiga mfano wa Hospitali hiyo.

 
"Mungu awasaidie na wilaya ya Rungwe ni moja kati ya wilaya
zinazowawezesha wenye ualbino kufika Hospitali ya Rufaa Mbeya kupata matibabu na vifaa" alisema Simwali.

 No comments: