Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, April 20, 2017

MAGEMU YATENGENEZA GENGE HATARI LA WATOTO MBEYABaadhi ya watoto waliokutwa na kamera yetu katika chumba cha siri cha mchezo huo mjini Mbalizi wilaya ya Mbeya.

Na Gordon Kalulunga

Kundi kubwa la watoto kati ya miaka 7-13 katika wilaya ya Mbeya mkoani hapa, wamejiingiza katika michezo hatari (kamali) za kiitwacho gemu ambapo kundi kubwa la wanafunzi hasa shule za Msingi wanaacha masomo na kujiunga na makundi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, imebainika.

Uchunguzi umebaini kuwa watoto hao wanaacha masomo na baadhi
wamejiingiza katika vitendo vya udokozi na wizi wa fedha majumbani
mwao ili kupata pesa za kulipia mchezo huo.

“Mchezo huu usije mruhusu mtoto wako wa shule aujue maana hata shule hatoweza kwenda na hapa tunawalipisha Shilingi 200 kila baada ya dakika 10” anasema mmoja wa wamiliki wa chumba cha siri cha biashara hiyo isiyolipiwa kodi.

Kamali hiyo hatari kwa watoto, kwa sasa imeanza kushamili kwa kasi
katika mji mdogo wa Mbalizi yakiwemo maeneo ya stendi ya tarafani na Mtakuja karibu na kambi ya Jeshi la wananchi wa Tanzania.

Kutokana na serikali kutoweza kuona athari hizo mapema, genge kubwa la watoto hao hasa wa kiume limeendelea kuongezeka na kuunda makundi maalum ya vituo vya kuchezea kamali hiyo na kupelekea kuwa na watoto
wengi wa mtaani ambao ni hatari kwa Taifa na kwa familia hasa pale
wizi unapoendelea kukomaa na makundi hayo kuendelea kuongezeka na watoto hao kuongezeka kwa kimo na umri.

Baadhi ya wananchi ambao wameendelea kuwa mashuhuda wa kamali hizo kwa watoto walipohijiwa walisema kuwa wanasubiri serikali ndiyo ichukue hatua maana wao wanaogopa kuingilia biashara za watu na uhasama kati yao na wachezesha kamali hizo licha ya kukiri kuwa udokozi umezidi majumbani mwao kwa wale wenye watoto wanaocheza mchezo huo.

Tathmini ya ripoti ya MDGs inaonesha kwamba serikali ilidhamiria
kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2015, hakuna mwanafunzi wa shule ya msingi ambaye angekatiza masomo.

Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2009 pia inaainisha umuhimu wa kuwepo marekebisho ili kufikia usawa wa kijinsia katika ngazi zote za elimu na mafunzo ikizingatiwa kwamba ushiriki wa wasichana ngazi ya elimu ya sekondari kwenda ngazi ya juu ni mdogo ikilinganisha na wavulana.

Sera inaelekeza kuweka utaratibu wa kuwabaini na kuchukua hatua dhidi ya watu watakaosababisha wanafunzi wa kike kukatisha masomo yao kwasababu yoyote ile; iwe utoro, kufanyishwa kazi ngumu na ujauzito.

No comments: