Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Monday, May 22, 2017

HOFU YATANDA FEDHA ZA RUZUKU YA ELIMU BURE MBEYANA GORDON KALULUNGA

FEDHA za ruzuku zinazotolewa na serikali kwa ajili ya uendeshaji wa shule kote nchini, zimezua hofu kwa baadhi ya wakuu wa shule baada ya matumizi yake kutowekwa wazi kinyume na waraka wa serikali unaowataka walimu wakuu na wakuu wa shule kuchangia asilimia 10. Imebainika.

Fedha hizo maarufu kama Capitation Grant zinazopelekwa moja kwa moja katika shule za Msingi na Sekondari zimegawanywa katika makundi matano.

Makundi hayo yanajumuisha asilimi 30 ya fedha hiyo inayopaswa kutumika katika ukarabati, asilimia 30 vifaa, asilimia 20 mitihani, asilimia 10 utawala na asilimia 10 kwa ajili ya michezo.

Katika Halmashauri hiyo baadhi ya walimu wamelalamikia hatua ya viongozi wa wilaya hiyo kuwalazimisha kutoa zaidi ya asilimia 10 kwa ajili ya michezo tangu mwaka jana2016, hali ambayo imewapelekea kuandika barua ya wazi kwa Rais Dkt. John Magufuli ili aingilie kati.

“Kwa shule za Msingi Serikali imekuwa ikitoa Tsh 536.40 kwa kila mwanafunzi kwa mwezi kwa ajili ya uendeshaji wa shule na hiyo fedha inatumika kwa mujibu wa waraka uliotolewa mwaka 2016 ambapo asilimia 10 ya shilingi 536.40 ni sawa na Tsh 600 na siyo Tsh. 1,000 kama tunavyolazimishwa sasa” imesema moja ya sentensi ya barua ya wazi kwa Rais Magufuli.

Uchunguzi umebaini kuwa kutokana na hali hiyo, fedha hizo za michezo hupelekwa katika shule ya Msingi Mtakuja ambayo inamiliki akaunti 61003700152 ambayo ipo katika benki ya Nationa Microfinance Bank (NMB).

Hata hivyo uchunguzi zaidi umebaini kuwa mabadiliko hayo yalianza kupitia barua ya tarehe 03.05.2017 kutoka ofisi ya Halmashauri hiyo ambayo ilikuwa ikielezwa kwa maafisa elimu Kata ya ikiwa na kumbukumbu namba MDC/E.10/34/49.

Barua hiyo ina kichwa cha habari kinachosomeka “MAREKEBISHO YA MASHINDANO YA UMITASHUMTA 2017” ambayo inaeleza kuwa walipokea barua kutoka ofisi ya mkoa wa Mbeya yenye kumb. DA.202./250/01/67 ya tarehe 24.04.2017 yenye kutoa maelekezo ya mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA.

“Marekebisho ya mchanganuo ni kama ifuatavyo, shule Tsh 100/=, Kata Tsh 150/=, Tarafa Tsh 200/=, Wilaya 250/=, Mkoa Tsh 300/= kwa kila mwanafunzi jumla yake Tsh 1,000/=” inasema barua hiyo ikiwasisitiza maafisa Elimu Kata kusimamia maagizo hayo.

Barua hiyo imewaeleza maafisa hao ngazi ya kata kuwa maagizo hayo yanazingatia mwongozo wa matumizi ya fedha hizo wenye kumbukumbu Na.DB.297/507/01/39 wa Desemba 28.2015 wa shule za Msingi na ule wa Sekondari Na.DB.297/507/01/40 wa Desemba 28 mwaka 2015.

Ofisa Habari wa wilaya ya Mbeya Hamza Mwangomale alikiri kuwepo malalamiko hayo ambayo alisema yanatokana na baadhi ya walimu kutumia maelekezo ya zamani tofauti na maelekezo mapya yaliyotolewa hivi karibuni.

“Utaratibu huu ni wa nchi nzima wala siyo hapa wilayani kwetu tu. Na suala la fedha hizo kupelekwa katika shule badala ya akaunti ya Halmashauri ni makubaliano yaliyofikiwa katika vikao ili kuepuka mlolongo wa watia saini wa Halsmashauri pindi zinapohitajika fedha hizo na wala siyo kwa nia ovu” alisema Mwangwala.

Baadhi ya walimu wa shule za Msingi na Sekondari katika wilaya hiyo walipohojiwa kwa makubaliano ya kutoandikwa majina yao, wamekiri kuwepo kwa hali hiyo na kwamba hata walipojaribu kupeleka malalamiko yao kwa maandishi walipuuzwa.

No comments: