Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, May 23, 2017

DIWANI MWANGOMALE AHAMASISHA MAENDELEO

 Diwani wa Kata ya Nsalala Jimbo la Mbeya Vijijini mkoani Mbeya akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Tunduma Road ndani ya Kata hiyo akihamasisha maendeleo.

 Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Mshikamano Kata ya Nsalala Jimbo la Mbeya Vijijini mkoani Mbeya, wakiwa kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na diwani wa Kata hiyo Mheshimiwa Kissman Mwangomale Leo, alipokuwa akipokea kero za wananchi na kuwapa mrejesho wananchi wa Kata hiyo mambo ambayo ameyatekeleza.
Picha zote na kikosi kazi cha Kalulunga blog.

WANANCHI wa kitongoji cha Tunduma Road, Ndola na Mshikamano Kata ya Nsalala Jimbo la Mbeya Vijijini mkoani hapa, wameunga mkono hoja ya diwani wa Kata hiyo Kissman Mwangomale (Chadema) ya kuchanga michango ya ujenzi wa vyumba Vinne vya madarasa katika shule ya Msingi Nsalala na Mapelele.


Hoja hiyo imetolewa leona diwani huyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji hicho alipokuwa akipeleka mrejesho wa kazi alizozifanya na kuchukua kero za wananchi pamoja na kujibu maswali yao.


Kiongozi huyo alisema awali wamefanikiwa kujenga matundu 16 ya vyoo katika shule hizo na kwamba ametekeleza ahadi ya kushughulikia suala la maji, miundombinu ya barabara na anajivunia kuhakikisha walimu waliopo katika shule zilizopo katika kata hiyo hawanyanyasiki.


“Nilitembelea katika shule hizo na kukuta wanafunzi wa chekechea wakiwa wamekaa chini ya mti hivyo nikaonana na wataalam kisha wakafanya mchanganuo ambao ujenzi utagharimu kiasi cha Shilingi Milioni 34, ninaomba kutoa hoja kwenu ili tuweze kuchangia Tsh. 10,000/= kwa kila mmoja wetu” alisema kiongozi huyo.

Wakichangia hoja katika mkutano huo, baadhi ya wananchi wa eneo hilo walimsifu kiongozi huyo kwa kuibua hoja hiyo.


“Huo ndiyo uongozi na ungekuwa kiongozi wa kushinda ofisini usingeweza kujionea kero kama hizo ikiwemo kero ya vyoo katika shule zetu” walisema wananchi hao wakiongozwa na Gervas Njeje na Hamis bdallah ambaye aliunga mkono hoja na kuzungumzia kero ya taka katika Mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi.


Kwa mujibu wa diwani wa kata hiyo, alisema kuwa Halmashauri ya wilaya hiyo inatumia asilimia 6 ya mahitaji yake kutokana na kuwa na mapato ya Bilioni 2.5 kwa mwezi badala ya asilimia 44.

No comments: