Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Saturday, May 27, 2017

WAKENYA WAISHI NCHINI KWA KUBADILI MAJINA

Na Charles Ndagulla, Kalulunga Blog Moshi

MKUU  wa wilaya ya Mwanga,Aaron Mbogho,ameonya raia wa nchi za kigeni wanaoishi hapa nchini isivyo halali kwamba watakamatwa mara moja na kurejeshwa makwao na kuwataka wananchi kuwafichua wote wanaoishi bila kufuata sheria za nchini.

Hatua hii inatokana na kuwepo na raia wa Kenya wanaoshi nchini kinyume na sheria za nchi na kujichimbia katika vijiji vilivyopo mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Uchunguzi umebaini kuwa,baadhi ya raia hao wa Kenya wanaishi na kuendesha biashara kubwa katika maeneo ya mipakani isivyo halali huku baadhi ya viongozi wa vijiji vilivyopo mipakani wakidaiwa kuwasaidia raia hao kuingizwa kwenye daftari la kudumu wapiga kura.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni,mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa mtu yeyote anayeishi nchini bila kibali wala nyaraka mhimu za kuonyesha uhalali wa kuwepo hapa nchini huyo ni sawa na wahamiaji haramu.

Mkuu huyo wa wilaya amekiri kuwepo na viongozi wa vijiji vilviyopo mpakani kuwasaidia raia wa kigeni kuishi nchini kinyemela na kuonya kuwa viongozi watakaobainika kuwalinda raia hao watachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Tukidhibitisha kuwa huyo mtu siyo raia wa Tanzania na hana nyaraka zozote za kuishi hapa nchini tunamrudisha kwao,mhimu hapa ni kudhibitisha kama kweli si raia wa Tanzania”,alisema.

Baadhi ya raia hao kutoka nchini Kenya wamebuni mbinu mpya ya kuishi nchini kwa kubadilisha majina yao ya asili ya Kenya na makabila yao na kutumia majina ya makabila ya hapa nchini.

Mmoja wa raia wa Kenya kutoka Taveta aliyeingia nchini akiwa na umri wa miaka kati ya 17 na 20 akijishugulisha na shughuli za vibarua kwenye mashamba ya watanzania, amebadilisha jina lake la asili na kujipachika jina la kipare.

Raia huyo amejikuwa ajitambulisha kwa jina la Steven Mrutu akidai ni mpare kutoka kijiji cha Mnoa wilaya ya mwanga kijiji ambacho kipo mita 100 kutoka eneo la kitobo nchini Kenya.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi,raia huyo wa Kenya aliyejitambulisha kwa jina la Steven Mrutu, alidai kuwa yeye ni mzaliwa wa kijiji hicho cha Mnoa huku mke wake ambaye pia ni raia wa Kenya akidai amezaliwa eneo la Kilototoni wilaya ya Moshi Vijijini.

Hata hivyo baada ya kubanwa kwa maswali na mwandishi wa habari hizi alimuomba mwandishi kutoandika habari hizo huku akisisitiza kuonana na mwandishi ahadi ambayo alishindwa kuitekeleza hadi sasa.

“Mimi ni mtanzania nimezaliwa hapo Mnoa lakini naomba usiandike kwanza hizi habari mpaka tuonane haya ni maneno ya uongo yanazushwa na wabaya wangu”,alisema .

Raia huyo wa Kenya ambaye amesajili laini zake za simu kwa majina ya kipare, amekuwa akiwaingiza nchini ndugu zake  kutoka nchini Kenya na kuwasaidia kupata vitambulisho vya ukaazi kwa msaada wa maofisa watendaji wa vijiji vilivyopo mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Wakati raia huyo akidai ni mtanzania anayehsi kijiji cha Mnoa,uchunguzi wetu umedhibitisha bila kuacha shaka kuwa raia huyo  anyefahamika  na wengi kwa jina la  Fikiri,anaishi eneo la Chekereni katika kijiji cha Ghona kilichopo kata ya Kahe Mashariki wilaya ya Moshi Vijijini na si kijiji cha Mnoa wilaya ya mwanga kama anavyodai.

No comments: