Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, May 03, 2017

Wanahabari Mbeya wawaalika wadau wa habari kushiriki siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani

MWENYEKITI wa chama cha wandishi wa habari Mkoa wa Mbeya (MBPC), Modest Nkulu, amewataka wananch wanaoishi mkoani humo wajitokeze kwa wingi leo May 3,2017 kuungana na wanahabari wa mkoa huo katika kuzijadili changamoto zinazowakabili wanahabari nchini.

Rai hiyo ameitoa katika mahojiano maalum na Mwandishi wa Kalulunga Blog na kwamba licha ya changamoto zinazoonekana kuwakabili wanahabari lakini pia kuna mafanikio yaliyotokana na kazi za wanahabari.

"Kauli mbiu ni Klabu za waandishi wa habari zina wajibu wa kuendeleza amani katika jamii" alisema Nkulu.

Kabla ya kwenda kujadili na kukutana na wadau wa habari mkoani hapa, jioni ya leo kutakuwa na michezo katika uwanja wa chuo cha uhasibu (TIA) tawi a Mbeya na baadae kukusanyika katika ukumbi wa Mtnda uliopo Soweto Jijini Mbeya.


No comments: