Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, May 25, 2017

WANAWAKE WADAIWA KUNYANG'ANYWA KUNI VICHWANI
Na Gordon Kalulunga, Mbeya

WANAWAKE wanaoishi katika Kata ya Nsalala wilaya ya Mbeya mkoani hapa, wameilalamikia serikali kuwa inawanyanyasa kwa kuwanyang’anya kuni vichwani pindi wanaporudi majumbani kwao wakitoka kutafuta kuni za kupikia majumbani kwenye vichaka.

Malalamiko hayo waliyatoa mbele ya diwani wao Kissman Mwangomale (Chadema), alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kuhamasisha maendejana.

Mmoja wa wanawake aliyejitambulisha kwa jina la Pona Nambene, huku akishangiliwa na wanawake wenzake, alisema jambo hilo limekuwa kero kubwa kwa wanawake wa Kata hiyo ambayo haipakani na pori lolote tengefu.

“Naomba tushirikiane kupaza sauti zetu kuondoa kero za watu wa Maliasili ambao wanatupora wanawake kuni wakidai ni mali yao na tukifanya biashara ndogondogo ushuru juu na tukiopoa mchanga mtoni tunakatazwa, serikali inatunyanyasa sana” alisema mwanamke huyo huku akishangiliwa kila alipozungumza.

Akijibu kero hiyo, diwani Mwangomale awali ya yote alisema anaomba sana vyombo vya habari vishirikiane naye pamoja na wananchi kupaza sauti juu ya kero zao ili viongozi wakuu wa serikali wapate kuyajua yanayoendelea vijijini.

“Kalulunga na waandishi wengine naamini hamtawaangusha wananchi hawa maana kuna sheria zingine hata tukihoji Halmashauri majibu tunayoyapata tunajibiwa kuwa sheria hizi zilitungwa na madiwani waliopita wenye hadhi kama sisi” alisema diwani huyo.

Kuhusu kero ya uchafu ambayo wananchi walilalamikia taka kuzagaa katika mitaa yao, alisema kuwa maamuzi ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mnasa Nyerembe ndiyo yamesababisha hali mbaya ya uchafu kuendelea kuzagaa.

“Maamuzi ya kukurupuka ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya kuamua kuvunjwa kwa maghuba ndiyo yametufikisha hapa na niwaambie ukweli wananchi kuwa Halmashauri yetu ya Mbeya ina trekta moja tu kwa ajili ya usafi wa wilaya nzima” alisema Mwangomale.

Katika ziara hiyo, aliwaambia wananchi jinsi gani alivyotekeleza ujenzi wa barabara na maji mpaka sasa ambapo serikali inatarajia kupeleka Shilingi Milioni Mia Tatu kwa ajili ya mradi wa maji.

No comments: