Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Friday, June 16, 2017

KACHERO; KUNA MAKUNDI HATARI KULIKO LOWASSAKachero mstaafu Said Salimin Said (kulia), akiwa anahojiwa na Mwandishi wa habari Gordon Kalulunga mjini Mbeya hivi karibuni.

NA GODON KALULUNGA

KACHERO mstaafu wa idara ya usalama wa Taifa Said Salimin Said amesema kuwa kuna makundi hatari zaidi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuliko kundi dogo la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Edward Lowassa.Hayo aliyasema mwishoni mwa wiki katika mahojiano maalum na Mwandishi wa habari hii mjini Mbeya katika kuelekea uchaguzi wa ndani wa CCM ngazi ya wilaya na mikoa.Kachero huyo alisema kuwa watanzania wengi hawajui kuwa marais wa Tanzania wa awamu ya kwanza mpaka awamu ya tatu Benjamin Mkapa hawakupatikana kutoka katika makundi ndani ya chama.“Ngoja nikuambie buana, ni Rais Kikwete pekee ambaye alitokana na kundi la Lowassa ambaye alikuwa na matarajio yake ya kupata urais 2015 na baada ya Lowassa akuondoka kuna mitandao miwili mibaya kuliko mtandao mdogo aliouacha Lowassa ndani ya chama” alisema Said Salmin.Kiongozi huyo ambaye pia anatajwa kuwa anaweza kujitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho mkoa wa Mbeya alisema yeye ni kiongozi mwenye mawazo huru (Free thinker) hivyo kama atawania nafasi hiyo na kushinda atapiga vita makundi ambayo yanazalisha rushwa.


“Mimi ni mpenzi wa vijana wote hasa vijana ambao siyo wala rushwa, siyo unakuwa na vijana wala rushwa wanaopenda wafanikiwe haraka na hao baadhi yao ndiyo wanaolalamikia serikali kuwa kwanini hawateuliwi katika nafasi mbalimbali. Nitapiga vita rushwa kwenye chaguzi” alisema kiongozi huyo.Alisema kwa mkoa wa Mbeya kitu kinachopungua na kinatakiwa kifanyike kwa chama hicho ni juhudi kubwa za kuongeza wanachama hasa vijana ambao wanapaswa kufundishwa sera na ilani maana ndiyo msingi wa maendeleo.“Vijana wengi wala rushwa walienda vyama vya upinzani kwasababu ya tamaa ya kufanikiwa haraka bila kujua kuwa maendeleo ni hatua kama za mtoto anapozaliwa, nawashauri warejee ndani ya CCM na wana CCM wachague viongozi waadilifu” alisema kachero huyo.Alipoulizwa kama atawania nafasi hiyo anayotajwa alisema kuwa wakati ukifika na chama kikifungua milango kwa wanaotajwa na wasiotajwa kujitokeza kusema atasema.

No comments: