Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Monday, June 05, 2017

MANGULA KUTEMBELEA WILAYA ZINAZOTAJWA KUWA SUGU KWA UBADHILIFU

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Philip Mangula (Pichani), ameanza ziara yake ya siku tatu leo mkoani Mbeya.

Mangula ambaye pia ni mlezi wa chama hicho mkoa wa Mbeya, anatarajia kutembelea wilaya za Kyela, Mbeya Vijijini na Mbeya Mjini.

Taarifa zinasema kuwa ziara ya kiongozi huyo zinalenga kupata ukweli wa mwenendo wa chama na serikali ambapo wilaya hizo zinatajwa kuwa na migogoro ya kisiasa na ubadhilifu wa fedha za chama hicho na hata ndani ya serikali.

Mbali na viongozi wa chama hicho kuitisha kamati za siasa ili kuweza kuweka msimamo wa mambo ambayo anapaswa kuelezwa kiongozi huyo ili kumwaminisha kuwa hali ni shwari, taarifa zinasema kuwa kuna baadhi ya wajumbe ambao wameapa kusema ukweli mbele ya Mangula licha ya kukubaliana katika vikao kumdanganya.

Hali ya kisiasa kwa CCM katika wilaya hizo inazidi kudidimia kutokana na migongano na ubadhilifu katika baadhi ya Halmashauri. 

Hata hivyo imeelezwa kuwa ziara ya Mangula inaweza kuwa chachu ya kukikomboa chama hicho katika chaguzi zijazo kuanzia uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu 2020 au kuujua ukweli wa matokeo tarajali katika chaguzi hizo zijazo.

 

No comments: