Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, June 20, 2017

MCHUNGAJI AMPACHIKA MIMBA MWANAFUNZI
MCHUNGAJI wa kanisa la Jeshi la wokovu mkoani Mbeya James Mwita ambaye ni Mkurugenzi wa shule ya sekondari Itundu iliyopo wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani hapa, anadaiwa kufanya ngono na mwanafunzi Happy Fredy wa kidato cha tatu wa shule hiyo kisha kumpachika mimba.

Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya walimu wa shule hiyo, zimesema kuwa baada ya kubainika kuwa mwanafunzi huyo anaujauzito, kiongozi huyo wa kiroho aliamua kutoroka ili kujificha na aibu hiyo.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii kwa njia ya simu, mkuu wa shule hiyo Mwalimu Gabriel Mwansiha, alishindwa kuthibitisha wala kukanusha kuwepo kwa tukio hilo.

“Ili kuweza kuzipata vizuri habari hizi naomba ufiki ofisini maana tutakuwepo wengi na hata kama mimi sintakuwepo atakuwepo msaidizi wangu” alisema Mwalimu Mwansiha.

Mtuhumiwa alipotafutwa kwa namba zake za simu ya kiganjani hakuweza kupatikana na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi hakuweza kuujibu kwa muda wa siku mbili.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo William Simwali, alisema alitaarifiwa na Katibu wake ambaye ni Mkuu wa shule hiyo kuhusiana na suala hilo hivyo ameagiza mwalimu aitishe haraka kikao cha bodi ya shule.

“Sisi mtumishi yeyote akituhumiwa kwa kashfa kama hii ya huyu kiongozi lazima aondolewe shuleni na hii ni kuiondolea shule aibu na kurejesha utulivu shuleni” alisema Simwali.

Kuhusu Mwanafunzi alisema shule kwasababu moja ya sheria za shule ni mwanafunzi kufukuzwa akibainika anafanya ngono shuleni au kupata ujauzito.

Askofu wa Jeshi la Wokovu Ilembo Daniel Simwali, ambaye ni msimamizi wa mchungaji huyo alisema wao tayari wamechukua hatua ya kumvua uchungaji na kumfukuza kabisa.

"Kwanza alitoroka baada ya taarifa kuvuja na kufunga simu zake zote. Tyumemtafuta bila mafanikio hivyo tumemvua uchungaji na kumfukuza kazi na hata familia yake hatukuweza kuipa hata senti hivyo siyo mchungaji wetu tena" alisema Askofu huyo.
Mratibu wa kitengo cha uzazi wa mama na mtoto mkoani Mbeya Prisca Butuyuyu amesema kuwa utafiti wa mwaka 2010 unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 23 ya wasichana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 19 walipata mimba na mwaka 2015 idadi iliongezeka na kufikia asilimia 27.

“Mwaka 2016 Mkoa wa Mbeya pekee ulilipotiwa kuwa na vifo 94 vya wajawazito na kati yao 27 sawa na asilimia 31 walikuwa ni wasichana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 vifo ambavyo vilisababishwa na kuishiwa damu, kifafa cha mimba, maralia na vichomi” alisema Butuyuyu.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Mariam Mtunguja alisema kuhusu maambukizi ya VVU kwa vijana wenye umri kati ya miaka 13 hadi 24 Tanzania ni asilimia 3.3 huku Mkoa wa Mbeya pekee wakiwa asilimia 6.3 hali ambayo ni hatari kwa vijana wadogo.

Katika ripoti ya utafiti wa Demografia na afya ya mwaka 2010 (DHS) inaonyesha kwamba ni asilimia 25 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa ambao wangependa kupumzika, kupangilia uzazi, lakini hawatumii njia zozote za uzazi.


No comments: