Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, June 22, 2017

RC MAKALLA AONYESHA UGWIJI WA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI
MKUU wa mkoa wa Mbeya nchini Tanzania Amos Gabriel Makalla, ameonyesha umahiri wake wa kusikiliza wananchi na kumaliza migogoro ya ardhi mkoani humo.

Leo mkuu huyo wa mkoa amemaliza mgogoro wa muda mrefu wa shamba la serikali la LANGWILA lililopo wilayani Mbarali lenye ukubwa wa Ekari 735.

Shamba hili lipo chini ya wizara YA kilimo na kwasasa linatumika kuzalisha nyasi na ni ekari 100 tu zinazotumika.

Ameruhusu wananchi kulima shamba hilo lkiwa utaratibu maalumu wa kusajiliwa na uongozi wa kijiji na kuwasilisha majina hayo kwa uongozi wa shamba ambao kisheria ndiyo wamiliki halali.

Uamuzi huo umezingatia upungufu wa ardhi uliopo ktk Kijiji cha Mhwela na maeneo mengine mengi kata YA Mwatenga.

Amewaonya wananchi kutokukodisha maeneo yao walionayo ili kukimbilia shamba la serikali na hivyo ameagiza uhakiki ufanyike kubaini wasio na ardhi apatiwe maeneo YA kulima kwa utaratibu maalum.

- Aidha amewashauri uongozi wa kijiji , kata na wilaya kuomba sehemu YA shamba hilo ili awasilishe mamlaka YA juu.

No comments: