Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, June 29, 2017

WALAJI CCM KULAZWA NJAA
Mwenyekiti mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Amkeni  lililopo mjini Mbalizi wilaya ya Mbeya mkoani hapa Anganile Mwambuluma, amesema mwisho wa walaji wa mali ya chama hicho umefika.

Aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za tawi hilo na kwamba anaanza na mambo matatu ambayo yatakisaidia chama hicho kishinde uchaguzi wa mitaa mwaka 2019.

“Kwanza kabisa naanza na suala la miradi ya chama katika tawi letu ambayo umefika wakati wa wanachama wote kujua mapato na matumizi pamoja na kuwaunganisha viongozi na wanachama” alisema Mwambuluma.

Mikakati yake mingine aliitaja kuwa ni kuongeza wanachama wapya hasa vijana na kuitisha mikutano ya wanachama wote na kusikiliza kero zao na ushauri kwa ajili ya maendeleo ya chama na tawi hilo.

“Kwa ujana wangu vivyo hivyo mkakati wangu ni kuwarejesha vijana katika chama ikiwa ni pamoja na kuwapa mikakati ya kujiwezesha kupitia vikundi na kuwasimamia” alisema kiongozi huyo ambaye kikazi ni mpiga debe na Mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya Ushindi ya mjini Mbalizi.

Wakati uchaguzi wa chama hicho ngazi ya matawi ukiendelea kumalizika, fomu za kuwania nafasi za uongozi ngazi ya wilaya zinatarajiwa kuanza kutolewa mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu.

No comments: