Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, June 01, 2017

WATUMISHI 6 KYELA WASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA UBADHILIFUMBUNGE WA JIMBO LA KYELA MKOANI MBEYA DKT. HARISON MWAKYEMBE.
..........................................................................................................

WATUMISHI 6 wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Dr. Hunter Mwakifuna alisema kuwa Halmashauri imechukua hatua hiyo kutokana na taarifa kutoka Taasisi ya kupamabana na kuzuia rushwa (TAKUKURU) kuwa wameanza kuwachunguza watumishi hao.

Alisema tuhuma zinazowakabili zinahusiana na taratibu za utumishi wa umma ambapo wanatuhumiwa kufanya kazi za kihasibu bila kufuata taratibu za kifedha.

“Tuhuma zinazowakabili ni pamoja na matumizi ya fedha za uchaguzi zilizoletwa kwa ajili ya vifaa vya uchaguzi mwaka 2015 , pia kuna tuhuma za fedha mbichi ambazo hazikupita benki zilizotokana na makusanyo ya ushuru wa COCOA milioni 31 za mwaka 2015” alisema Mwakifuna.

alisema jumla ya watumishi wanaohusika na tuhuma hizo ni nane akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Clemence Kasongo ambaye amehamishiwa ofisi ya RAS Mbeya na aliyekuwa mweka hazina wa Halmashauri hiyo Alfa Baraza ambaye amehamishiwa Halmashauri ya Kilindi.

“Tulichokifanya tumewaandikia waajili wao wapya ili warudi kujibu tuhuma” alisema Mwenyekiti huyo.

Aliwataja wengine kuwa ni pamoja na Mweka hazina wa wilaya hiyo ndugu Muya, Pastory Nsemwa aliyehusika na makusanyo ya ndani, Omary Mungi, Chaka chaka, afisa usafirishaji Freedom Mwainunu na afisa mipango Francis Mwaipopo ambaye alikuwa kaimu Mkurugenzi na aliidhinisha fedha” alisema kiongozi huyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Benard Semwaiko alisema wajibu wake baada ya kupata taarifa kuwa wanachunguzwa na chombo cha kisheria, wajibu wake ni kuwasimamisha kazi

“Watumishi hawa hawaruhusiwi kutoka nje ya vituo vyao vya kazi na wataendelea kulipwa mishahara mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika” alisema Mkurugenzi huyo. 
  
Baadhi ya watuhumiwa walipotafutwa kwa njia ya simu zao za viganjani ili waweze kueleza mtazamo wao juu ya tuhuma hizo hawakupatikana.

No comments: