Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, August 09, 2017

BIOLAND WAGAWANA FAIDA NA WAKULIMA WA KAKAO BUSOKELOMkurugenzi wa kampuni ya KIM'S Chocolates ya nchini Ubelgiji, Fons Maex (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mbeya kuhusu mradi wa kujenga vyumba vya madarasa katika shule za Msingi wilayani Kyela na Rungwe mkoani Mbeya (SCHOOL PROJECT) chini ya kampuni hiyo na Biolands Tanzania. Katikati ni Mkuu wa Kampuni ya Biolands Tanzania, Frank Carl Peter Neumann na kulia ni Meneja wa oparesheni za kampuni ya Bioland Tanzania Felix Mtawa
 Shule ya Msingi Kingili iliyopo katika Halmashauri ya Busokelo Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.


NA GOIRDON KALULUNGA

KAMPUNI ya ununuzi wa zao la Kakao katika wilaya ya Rungwe na Kyela mkoani Mbeya ya Biolands International Ltd, imegawana faida za zao hilo na wananchi wa Halmashauri ya Busokelo Wilayani Rungwe kwa kujenga vyumba vya madarasa 9 na ofisi za walimu 2.

Madarasa na ofisi hizo vimejengwa katika shule tatu za Kingili, Ndobo
na Kasyabone ambapo vilikabidhiwa mwishoni mwa wiki kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhusri ya Muungano wa Tanzania Dkr. Tulia Ackson Mwansasu.

Katika hafla hiyo ya kukabidhi madarasa na ofisi hizo iliyofanyika
mwishoni mwa wiki, Meneja uendeshaji wa kampuni hiyo Felix Mtawa, alisema Jumla ya Shilingi Milioni 33, 349,469 zilitumika katika ujenzi huo ambao wameshirikiana na wananchi.

“Tangu mwanzo Bioland inafanya kazi na wakulima zaidi ya 9000 na kabla ya kampuni yetu soko la zao hili la kakao halikuwa la uhakika kwa wakulima hivyo jambo la kwanza tulianzisha uboreshaji wa Kakao na kuwafundisha wakulima ambao wameelimika na uzalishaji kwa sasa ni zaidi ya tani 9000 kwa mwaka wakati awali haikuzidi tani 3000” alisema Mtawa.

Mbali na hayo alisema kwa sasa awamu ya kwanza pekee wameweza
kukarabati jumla ya vyumba vya madarasa 13, ofisi za walimu 3 na vyoo vyenye matundu 8 katika shule ya Msingi Kipyola, Kibole na Ilamba walikotumia kiasi cha shilingi Milioni 16,772,842.

“Yanayofanyika yote ni miongoni mwa vipaumbele vyetu likiwemo suala la Elimu hasa elimu ya Msingi, Afya katika kuhamasisha jamii ya wakuilima kujiunga na Bima ya Afya ya jamii (CHF) na kuongeza uzalishaji wa zao la Kakao kwa kutoa mafunzo kwa wakulima” alisema Meneja huyo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Bioland Frank Nemann alisema kampuni hiyo itaendelea kufundisha wakulima mbinu mbalimbali za kilimo na kuendelea kusambaza miche ili kuongeza uzalishaji wenye tija kwa wakulima.

Naye mtendaji mkuu wa kampuni ya Kim’s Chocolates kutoka Ubelgiji Fons Maex aliwaomba wakulima kuendelea kuwauzia Kokoa yao Biolands ili yeye aweze kupata Kakao hiyo kwa wingi na kupata faida ambayo inatumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na kufanikisha mpango wa kujenga madarasa 1800 ifikapo mwaka 2023.

Naibu Spika Dkt. Tulia Mwansasu aliipongeza kampuni hiyo kwa kuweza kuona umuhimu wa kuijali jamii ambayo wanafanya nayo biashara na akawasisitiza wakulima kuendelea kuwauzia Bioland Kokoa huku akisisitiza kwa Lugha ya Kinyakyusa akisema “Abha bhu bhakamu bhitu bhule”

Aidha alisema kuwa Serikali hususani Bunge limesikia juu ya jambo hilo jema kwa jamii linalofanywa na kampuni hiyo.

Mkwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Busokelo Atupele Mwakibete alisema “Natoa pongezi kwa kampuni ya Bioland na Kim’s Chocolates International kwa kushirikiana na wananchi katika mpango wao wa kukarabati majengo na madarasa zaidi ya 400 katika jimbo langu hadi mwaka 2020” alisema Mwakibete.

No comments: