Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, August 06, 2017

WANG'ANG'ANIA IFISI HOSPITALI ILI WASIKATWE MIGUUWANG’ANG’ANIA IFISI HOSPITALI ILI WASIKATWE MIGUU

Mbeya.

MAJERUHI kadhaa waliopata ajali mkoani Mbeya na kulazwa katika Hospitali teule ya wilaya ya Mbeya Mbalizi Ifisi, wamekataa kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Mbeya kwa hofu ya kwenda kukatwa miguu yao.

Wakizungumza na waandishi wa habari ndani ya wodi namba 3 ya Hospitali hiyo inayomilikiwa na Kanisa la Uijilisti Tanzania kwa ubia na serikali, wamesema kuwa kuna baadhi ya wenzao walikatwa miguu baada ya kufikishwa katika Hospitali hiyo ya kanda.

“Mimi sitaki mnipeleke Rufaa wataenda kunikata miguu yangu, sitaki nawaomba maana kuna mwenzangu alipopelekwa huko alikatwa” alisema Mesia Sichone (28) mbele ya Katibu wa Hospitali hiyo Emmanuel Martin.

Dereva wa gari aina ya Coaster, Sai Mshani ambaye alipata ajali Agost 5, 2017 eneo la Mwembeni Kata ya Bonde la Songwe Mbeya Vijijini, aliwaambia waandishi wa habari Hospitalini hapo kuwa alipata huduma nzuri licha ya mguu wake kuvunjia mara mbili.

“Usiku nilikuwa Napata maumivu makali sana kichwani, kifuani na mkono wangu wa kulia lakini asubuhi ya leo naendelea vizuri umebakia mguu huu wa kulia ambao nimevunjika” 

“Yule dereva wa IT aliyapita magari kama sita hivi na nilipomuwashia taa akazidi kuja, sikuweza kupeleka gari korongoni ili kuua abiria nikaamua kusimama ndipo akatufuata. Tulitokea Tunduma kuja Mbeya” alisema dereva huyo.

Muuguzi mfawidhi wa Hospitali hiyo Elimati Sanga, alisema kuwa majeruhi wa ajali hiyo wengi wao wanaendelea vizuri na wale ambao hali zao hazitakuwa nzuri watawapeleka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na walipofikishwa hospitalini hapo timu nzima ya wataalam wakiongozwa na Mganga mkuu mfawidhi Dr. Martin waliwapokea na kuwaanzishia huduma.

Katibu wa Hospitali hiyo Emmanuel Martin, alisema katika ajali hiyo walipokea majeruhi 26 na mwili wa marehemu mmoja ambaye ni raia wa Zimbabwe aitwaye Emmanuel Poshelai.

Aliwataja majeruhi wengine kuwa ni Damali Samson (22) mkazi wa Ifisi, Yunis Singwa (27) mkazi wa Ileje, Mesia Sichone (28) mkazi wa Ilemi, Sai Mshani (36) mkazi wa Songwe, Jestina Mwambogo mkazi wa Senjele, Charles Madeni (21) mkazi wa Must Iyunga, Said Sangu (27) mkazi wa Songwe na Subira Kitaju (27) mkazi wa Vwawa.

Wengine ni Love Shadrack (25) mkazi wa Nsalala, Elisha Mwaikambo (45) mkazi wa Tukuyu, Majaliwa Nsangalufu (29) mkazi wa Tukuyu, Sofia Mgomango (58) mkazi wa Ikuti, Edina Bukuku (49) mkazi wa Mbalizi, Godfrey Gaspali (38) mkazi wa Ludewa ambaye walimwamishia katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya ambako alifariki dunia.

Mbali na hao pia majeruhi waliofikishwa katika hospitali hiyo ni Adolfu Mkunja (59) mkazi wa Uyole, Nehemia Kibona (22) mkazi wa Ifisi, Vincent Caoshi (28) mkazi wa Sumbawanga, France Komba (40) mkazi wa Sokomatola, Paulo Gambi (47) mkazi wa Iwambi, Joshua Mwakaje (18), Philimon Mwambeya mkazi wa Iyunga, Ambele Moses mkazi wa Forest, Doto Solomon mkazi wa Uyole, Amon Julius mkazi wa Mbozi, Sijali Abdallah mkazi wa Mwanjelwa na Peter Kilulu (30) mkazi wa Iyunga ambaye alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya ambako alifariki dunia.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Dr. Fredy Mbwanji alipoulizwa kuhusu hofu ya majeruhi kukataa kupelekwa katika Hospitali hiyo kwa madia ya kukithiri kwa ukataji wa viungo hususani miguu, alikanusha taarifa hizo.

"That's a myth, hakuna kitu kama hicho, mtu akikatwa mguu ni kwa sababu za kitalamu, shida huwa kuna denial na hii humtokea yeyote, bse kukatwa kiungo chako si jambo dogo" alijibu Dr. Mbwanji.

No comments: