Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, October 24, 2017

IFISI FC WAIDUNGA FELALI GOLI 3-0 LIGI DARAJA LA TATU MBEYA


NA GORDON KALULUNGA, MBEYA

Timu ya Ifisi Hospital FC ya Mbeya Vijijini inayoundwa na wafanyakazi wa Hospitali teule ya wilaya ya Mbeya, imeichapa goli 3 kwa nunge timu ya Felali FC ya Jijini Mbeya katika mchezo wao wa daraja la Tatu uliofanyika uga wa uwanja wa Jeshi mjini Mbalizi hapo jana.

Katika mtanange huo ambao ulivuta umati wa watazamaji uwanjani hapo sambamba na burudani za mbio za kujitolea kwa watu wanene, timu ya Ifisi iliibuka mshindi kwa magoli safi yaliyofungwa na wachezaji wa timu hiyo.

Goli la kwanza lilifungwa dakika ya 18 na mchezaji Richard Ng’ondya na baada ya dakika Nne tu yaani dakika ya 22, mchezaji Benjamin Dominic alitikisa nyavu za Felali baada ya kuuweka mpira safi gambani kisha kupiga shuti la kushitukiza.

Bao hilo lilisababisha mpira kusimama kwa dakika tatu kutokana na shuti la mfungaji huyo kufumua nyavu za lango la wapinzani wao.

Baada ya mapumziko na mpira kuanza tena, dakika ya 52 kelele zilisikika tena katika uwanja huo mithili ya shangwe za ushindi za mtu aliyekombolewa kutoka katika mikono ya watekaji.

Lilikuwa ni bao la 3 kwa timu ya Ifisi lililofungwa na mchezaji Frank Kavila maarufu kwa jina la Kidumu ambapo mpaka dakika 90 zinakwisha Felali walikuwa hawajaweza kuzigusa nyavu za Ifisi hata za pembeni ili kumtia moyo mwalimu wao.

No comments: