Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, October 22, 2017

IFISI FC MBEYA YAWAANDALIA SINDANO FELALI FC KESHO
NA GORDON KALULUNGA, MBEYAIFISI Hospitali FC ya Mbeya Vijijini inayoundwa na wafanyakazi wa Hospitali teule ya wilaya ya Mbeya, imesema imewaandalia sindano timu ya Felali ya Jijini Mbeya katika mchezo wao wa daraja la Tatu watakaokutana katika mtanange wa kuvutia utakaopigwa katika uga wa uwanja wa Jeshi mjini Mbalizi hapo kesho.Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo, Katibu wa Timu hiyo Nathaniel Christopher amesema kuwa wachezaji wa timu yake wapo timamu na wameahidi kuwa kesho kazi yao ni moja tu ya kuwatibu kisaidkolojia watani wao Felali FC kabla hawajawachoma sindano.Akitoa tambo hizo akiwa na Mwalimu msaidizi wa timu hiyo Faraja Ntima, amesema mashabiki wa timu hiyo wakiwemo baadhi ya wagonjwa wanaowatibu wasiwe na wasiwasi kwa madai kuwa ushindi katika mechi hiyo kwao ni lazima.“Tunaenda kupambana na timu yenye jina kubwa lakini haitatuweza kwasababu wachezaji wetu ni vijana wenye nguvu na wapo vizuri kisaikolojia na ikumbukwe kuwa kesho tunachezea uwanja wetu wa nyumbani hivyo mashabiki wajitokeze kuja kuona ufundi wetu wa pasi zilizoenda shule na magoli ya kisomi” amesema Nathaniel.Kwa upande wake Katibu wa Hospitali hiyo Emmanuel Martin amesema yeye kama kiongozi katika taasisi hiyo kazi yake ni moja tu ya kuwawezesha wachezaji na uongozi wa timu kuwa katika utimamu wa viungo na saikolojia huku shabaha kubwa nmahusiano jamii.
 

No comments: