Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Saturday, November 18, 2017

IFISI HOSPITALI YATINGA SITA BORA, TUKUYU STARS IMOKikosi cha timu ya Ifisi Hospital ya Mbeya.
 
NA GORDON KALULUNGA, MBEYA

BAADA ya mzunguko wa mechi za makundi ligi daraja la tatu mkoani Mbeya, timu ya Ifisi Hospital FC ya Mbeya Vijijini inayoundwa na wafanyakazi wa Hospitali teule ya wilaya ya Mbeya, imefanikiwa kutinga sita bora kuusaka ubingwa wa mkoa.

Timu hiyo ilifanikiwa kufikia hatua hiyo baada kuigagadua kwa magoli matatu kwa nunge timu ya Middle FC.

Katika kundi  B ambalo kulikuwa na timu 6 ambazo ni Middle FC, Machalo FC, Ilemi FC, Felali FC, Iduda FC na Ifisi yenyewe, ni timu mbili zimeweza kufuzu.

Mbali na Ifisi Hospital, timu nyingine ambayo imechomoza katika kundi hilo ni pamoja na timu ya Iduda FC ambapo mpaka tunaenda mitamboni taarifa zilitufikia kuwa pia timu ya Tukuyu Stars (Banyambala) pia imepenya katika kundi lao.

Katibu wa timu ya Ifisi Hospital FC, Nathaniel Christopher alisema baada ya kufikia hatua hiyo wanajifua zaidi kuhakikisha wanatwaa ubingwa.

“Nia yetu ni moja tu kuwapiga tutakaopangiwa nao na kisha kupanda daraja” alisema Nathaniel.

Katibu wa Hospitali hiyo Emmanuel Martin alisema kutokana na morali na nidhamu ya hali ya juu waliyoionyesha wachezaji wao anaamini hata katika mzunguko wa sita bora watashinda.

“Wachezaji wetu wana morali na wanadhihilisha kabisa kuwa ni timu ya wadunga sindano maana kila timu iliyokuja tuliidunga ni mechi mbili tu ndizo tulipoteza katika mzunguko wa makundi hivyo wapenzi wa soka watarajie makubwa zaidi” alisema kiongozi huyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ligi Mkoa wa Mbeya Mwalimu Dickson Sinkwembe alisema wanajiandaa sasa kupanga msimamo wa ligi ili timu mbili zilizofuzu katika kila kundi ziweze kucheza sita bora kupata bingwa wa mkoa.

No comments: