Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Friday, November 03, 2017

NDELE MWASELELA KUSOMESHA WATOTO 13 WALIOFANYA VIZURI DARASA LA SABA MBEYA

Mdau wa Maendeleo nchini Tanzania ndugu Ndele Mwaselela (mwenye skafu ya bendere ya Tanzania shingoni), akiwa na wanafunzi waliofanya vizuri mtihani wao wa darasa la saba mwaka huu kwa kupata daraja A kutoka katika Kata ya Iyela Jijini Mbeya ambao ameahidi kuwasomesha jijini Dar es Salaam.
Mratibu elimu Kata ya Iyela Jijini Mbeya, Mwalimu Dickson Sinkwembe akitoaneno katika Mkutano wa wazazi waliokusanyika kwenye hafla fupi ya kuwapongeza wanafunzi wa darasa la saba waliofanya vizuri na kupata daraja A kisha mdau wa Maendeleo Ndele Mwaselela kuahidi kuwasomesha jijini Dar Esalaam.

MDAU wa maendeleo nchini Tanzania ndugu Ndele Mwaselela ameahidi kuwasomesha watoto 13 waliopata wastani wa alama A katika masomo yao ya darasa la saba.

Amesema atawasomesha watoto hao kutoka Kata ya Iyela Jijini Mbeya kuanzia kidato cha kwanza mpaka chuo kikuu.

Aidha yeye kwa kushirikiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson Mwansasu wameahidi kujenga upya vyoo vya shule ya Msingi Nero na Mapambano Jijini Mbeya.

Ahadi hiyo imetolewa leo na ndugu Mwaselela katika hafla fupi ya kuwapatia zawadi wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya darasa la saba katika kata ya Iyela.

Mwaselela alisema kuwa taarifa ya uchakavu wa vyoo hivyo aliipata kupitia vyombo vya habari hivyo waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya wanapaswa kupongezwa na kwamba watahakikisha vinajengwa na kukamilika kwa wakati licha ya kuwepo tatizo hilo kwa miaka mitano.

Alisema ataendelea kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa vitendo.

Pia kwa niaba ya wadau  nchini  amempongeza Naibu Spika Dkt. Tulia kwa juhudi zake za kumsaidia  Rais katika kutimiza azma yake ya kuleta maendeleo kwa usawa na ustawi wa Watanzania wanyonge.

Kwa niaba ya Wazazi wengine, mzazi aliyejitambulisha kwa jina la Sarah Ndambo, amewashukuru kwa pamoja Naibu spika  Dkt Tulia Mwansansu na Ndele Mwaselela kwa jitihada zao wanazo zionyesha kwa jamii.

Kwa upande wake Ofisa Elimu wa Jiji la Mbeya Ally Abdallah ameshukuru kwa msaada kuwasomesha wanafunzi hao 13 waliopata wastani wa daraja A, na kushukuru kwa msaada wa kujengewa vyoo, katika  shule za Mapambano na Nero. 

Kwa niaba ya Wenyeviti wa Kamati za  shule Kata ya Iyela Ephaim Kiloni amesema kwa kushirikiana na wazazi watahakikisha wanakamilisha haraka uchimbaji wa mashimo ya vyoo ili kuwanusuru watoto na maradhi pia kuutumia vema msaada waliopewa ambapo hakuna mzazi atakayechangishwa fedha bali watatumia nguvu zao.

Hata hivyo pamoja na juhudi zinazofanywa na wadau wa maendeleo lakini mvutano wa kisiasa unaonyesha kuzorotesha maendeleo.

Katika Kata ya Iyela yenye zaidi ya watu 50,000, mpaka sasa haina Zahanati wala kituo cha Afya licha ya kuwa na Wawekezaji wengi zikiwemo benki mbalimbali hivyo kukwamisha sera ya Afya ya mwaka 2007 inayoelekeza kuwa kila Kijiji kinapaswa kuwa na Zahanati na kila Kata inapaswa kuwa na Kituo cha Afya.

Imeandikwa na timu ya waandishi wa habari wa Kalulunga Blog.

Endelea kuwa nasi kwa kubonyeza link yetu ya www.kalulunga.blogspot.com
 

No comments: