Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, December 07, 2017

MATEMA BEACH, FUKWE SALAMA TANZANIA

 

MKURUGENZI WA MAENDELEO YA KANISA LA UINJILISTI TANZANIA MCHUNGAJI MARCUS LEHNER.


 
Na Gordon Kalulunga, Mbeya.
 
MKOA WA MBEYA Umebeba vitongoji vingi vilivyo na utajili wa ardhi yenye vivutio machoni kwa watu.
 
Wageni waliopata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya wana ushuhuda mzito.
 
 Mkoa huu umebeba safu nyingi za milima iliyo sheheni rasilimali za urithi  tangu nyakati zile za watu wa kale, rasilimali hizo ni misitu mikubwa iliyo hifadhi wanyama na ndege wazuri wa kuvutia.
 
  Vilevile ni mkoa ulio bahatika kuandika historia ya maajabu ya ulimwengu tangu kudondoka kwa Kimondo kwenye ardhi ya bara la Afrika  katika wilaya ya mbozi  kwa sasa huitwa mkoa mpya wa Songwe uliomegwa kutoka mkoani Mbeya.
 
 Pia vipo vivutio vingine mbalimbali vinavyoipamba ramani ya mkoa huo kama vile mabwawa yenye matukio ya maajabu kwa mfano bwawa lililoko eneo la Masoko maarufu kwa jina la (Kisibha), jirani kabisa na kilele cha mlima Rungwe.
 
 Pia  ziwa Lake Ngozi na daraja la Mungu ni baadhi ya vivutio vinavyotengeneza historia ya pekee katika mkoa huu na kanda ya nyanda za juu kusini.
 
Mbali ya vivutio hivyo, Ziwa Nyasa ni miongoni mwa vivutio hivyo ambavyo watu kutoka mataifa mbalimbali hufika kujionea ziwa hilo lenye hadhi kubwa katika bara la Afrika na samaki watamu.
 
Wageni mbalimbali hufika wilayani Kyela kujionea mandhali ya ziwa hilo ambalo linashika nafasi ya Tatu kwa ukubwa kati ya maziwa yaliyopo katika bara la Afrika.
 
Ziwa hilo pia linazihudumia nchi za Malawi , Msumbiji, na Tanzania yenyewe.
 
 Wananchi wa nchi hizo na wageni wengine wamekuwa wakinufaika na ziwa nyasa kwa uvuvi wa samaki  na viumbe wengine waishio majini kwa ajili ya chakula na biashara.
 
Kuwepo kwa mawasiliano kati ya Mbamba bey na Itungi Port pia ni sehemu ya faida.
 
Lakini kikubwa zaidi cha kujivunia katika kanda ya nyanda za juu kusini ni kuwepo kwa pango la “Matema Lake Shore Resort” Hoteli ambayo imeboresha mazingira ya ufukwe wa matema na kuwa sehemu ya kuvutia machoni pa wageni wanaofika eneo hilo .
 
Ni eneo tulivu lenye mandhali ya mimea ya rangi ya kijani kibichi limepambwa na safu za milima yenye kusheheni misitu ambamo hupatikana ndege wazuri  wa angani na mavazi ya wageni wanaotembelea hotelini hapo.
 
Matema Lake  shore resort ni eneo la pekee katika mwambao wa ziwa Nyasa, Eneo lililokuwa pori lakini sasa limegeuka kuwa lulu na kuwa makazi ya watu wenye jukumu la kujichanganya na makabila tofauti ya ndani na nje ya nchi.
 
Eneo hilo limejaa utulivu huku likisikika sauti za ndege  na kupwa kwa maji ya ziwa, hali ambayo baadhi   ya wageni  waliowahi kutembelea eneo hilo wanadiliki kulifananisha na bustani ya Hedeni.
 
Kanisa la uinjilisti Tanzania lenye makao yake makuu Mbalizi nje kidogo ya jiji la Mbeya  ndiyo chanzo cha kuwepo Lake Shore Resort.
 
Mkurugenzi wa maendeleo ya kanisa hilo Mchungaji Marcus Lehner anasema kanisa la Uinjilist lilifanya utafiti na kugundua kuwa eneo hilo linafaa kuweka vivutio ili kuiunga mkono Serikali katika jitihada za kukuza sekta ya utalii nchini.
 
Anasema kuwa, mafanikio ya kuwepo kwa kivutio hicho yanatokana na juhudi za kanisa hilo kwa kupitia wafadhili wake huku likipigania utunzaji wa mazingira.
 
Mchungaji Lehner anaeleza kwamba utafiti uliofanywa pia ulizingatia kuwepo kwa eneo zuri la kuogelea lenye mchanga safi na mzuri.
 
Mbali na hayo anafafanua kuwa Lake  shore resort inatoa huduma za chakula cha asili na kulala kinachoandaliwa kwa muda maalum ( order) pia ina nyumba mbalimbali zenye jumla ya vyumba 22 vikiwemo vyumba vya kujihudumia (self contained) Vipi vyumba vilivyo na vitanda kati ya viwili na vitano  (double-beds up to 5-beds).
 
Zipo  pia nyumba za ghorofa zinazo muwezesha mgeni kulitizama vizuri ziwa, lilivyo na umbo lake kabla ya kutumia usafiri wa boti au ule wa miguu na gari  (Landrover) huduma ambazo pia hupatikana pamoja na safari za kuelekea mwambao wa ufinyanzi.
 
Ziwa lina upana wa wastani wa kilomita 60 na urefu wa wastani wa kilomita 550 lina zaidi ya mita za kina kwenye mfumo wa bonde la ufa Afrika mashariki katika ujazo wa mita 500 kutoka usawa wa bahari
 
Matema ufukwe wake  pia unapambwa na safu za mlima Livingstone wenye urefu wa mita 3000. Wakazi wa eneo hili ni kabila la wanyakyusa ambao pia wanajulikana ka wangonde.
 
Kilomita tano kuelekea kusini katika mwambao huo huko linaishi kabila dogo la wakisi ambao wanajishughulisha na zaidi na biashara ya ufinyanzi.
 
Kwa ujumla unapofika matema , ukiangalia upande wa Kaskazini kuelekea kusini unaweza kufurahia umbo zuri la eneo hilo linalofananishwa na Bustani ya Edeni.

No comments: