Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Monday, February 19, 2018

IFISI HOSPITAL FC WAICHIMBA MKWARA TUKUYU STARS
NA GORDON KALULUNGA, MBEYATIMU ya Ifisi Hospital FC (Wadunga sindano) yenye maskani yake Mbalizi Mbeya Vijijini, imeitumia salamu timu kongwe ya Tukuyu Stars (Banyambala) kuwa itapandia daraja mikononi mwake hapo Februari 25, mwaka huu.Tambo hizo zimetolewa na Katibu wa Hospitali teule ya wilaya ya Mbeya Emmanuel Martin alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana na kutoa mwenendo wa timu yake ambayo imeweka kambi nje kidogo mwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe International Airport.“Juzi tumewanyuka Ilomba goli 5 kwa nunge hivyo hizi mechi mbili ya Syukula na Tukuyu Stars hazitupi pressure tutazidunga sindano na kupanda daraja hata kama Tukuyu wana udhamini wa wakubwa sisi tutaenda kuwafundisha soka ” alisema Emmanuel Martin.Timu hizo zinatarajia kuonyesha mtanange wa nguvu huko mjini Tukuyu wilayani Rungwe katika hitimisho la Daraja la Tatu ngazi ya 6 bora ambapo kati ya timu sita ni timu moja inatarajia kupanda daraja na kwenda daraja la Pili.Kesho timu hizo zinaingia katika viwanja tofauti ambapo Ifisi Hospital FC itacheza na timu ya Syukula ya wilayani Rungwe katika uga wa Sokoine ikiwa na Pointi 7 huku wakongwe Tukuyu Stars watawakaribisha timu ya Iduda (Timu ya Kijiji) kutoka Uyole katika uwanja wa Tandale mjini Tukuyu wakiwa na Pointi 6.Baada ya mechi hiyo, ndipo timu ya Ifisi na Tukuyu watakutana huku timu ya Iduda ikiwa na Pointi 7 kama Ifisi na timu ya Ilomba ikishika mkia chini ya timu za Yoso na Syukula.

No comments: