Mashabiki mbalimbal;i wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Tandale mjini Tukuyu.(Picha kwa hisani ya dinaismail.blogspot.com)
*Tukuyu
wangoja majaliwa kupanda daraja
* Ifisi yasubiri
suluhu
NA GORDON
KALULUNGA, RUNGWE
LIGI daraja
la Tatu ngazi ya Mkoa wa Mbeya hatua ya timu sita bora, inatarajiwa kutia nanga
kesho katika viwanja mbalimbali huku ubingwa ukinukia kwa timu mbili ambazo ni
Tukuyu Star (Banyambala) na Ifisi Hospital FC (Wadunga Sindano).
Mechi hiyo
ambayo inatarajiwa kupigwa kesho katika uwanja wa Tandale uliopo mjini Tukuyu
wilayani hapa, imekuwa gumzo katika mitaa mbalimbali ya wilayani Rungwe vikiwemo
vijiwe kadhaa katikati ya mji huu wa Tukuyu.
Timu ya
Tukuyu Star ili kupata ubingwa huo wa Mkoa wa Mbeya, inahitaji kuifunga timu ya Ifisi ambayo ina pointi 10 dhidi ya pointi 9 za wenyeji Tukuyu
Star.
Wakati wenyeji
Tukuyu wakiwa wanafanya kila aina ya ufundi wa kuweza kushinda mechi hiyo ya
kesho, timu ya Ifisi FC wao wanahitaji kupata suluhu ya aina yeyote kisha
kubeba ubingwa huo na kupanda daraja kuelekea daraja la pili.
Wachezaji wa
timu ya Ifisi ambao tayari wametinga mjini Tukuyu jana, leo asubuhi wameonekana
katika uwanja wa Katumba Two ambako taarifa zisizorasmi zinasema kuwa mtanange
wa timu hizo unaweza kuhamishiwa katika uwanja huo kutoka Tandale.
Mpaka sasa
msimamo wa ligi hiyo inajiweka wazi kuwa Ifisi Hospital FC ina pointi 7, Tukuyu
Star pointi 9, Iduda FC pointi 7, Yosso FC pointi 3, Syukula FC pointi 3 na
Ilomba FC pointi 0.
No comments:
Post a Comment