BUSU LA TIMIDA FYANDOMO KWA MHITAJI MBEYA


Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa kutoka mkoa wa Mbeya Cde.Timida Fyandomo ametembelea eneo la ujenzi wa nyumba ya muhitaji anayejengewa na taasisi ya Tulia Trust katika kata ya Iganjo Mbeya Mjini.


Akiwa katika eneo hilo Timida ameahidi kutoa Godoro kumsaidia muhitaji huyo ikiwa ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wake ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mhe. Dr. Tulia Ackson. 


Nyumba hiyo inayojengwa kupitia mpango wa Tulia Trust Mtaani Kwatu inatarajiwa kukabidhiwa kwa mlengwa huyo mapema Mwezi wa Nne(4) .

Post a Comment

0 Comments