29, Novemba, 2024
Ofisi ya Mbunge Jimbo la Lupa Chunya imeshiriki katika bonanza la C.W.T Mkoa wa Mbeya lililofanyikia Viwanja vya Sinjilili Chunya ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mh.Alhaji Mbaraka Batenga Mkuu wa Wilaya Chunya kupitia tukio hilo Mh.Masache Kasaka kupitia Katibu wake wa Jimbo Ndugu Zakaria Japhet Lawa na Katibu Msaidizi wa Tarafa ya kiwanja Ndugu Mpoki Mwakyusa waliweza kutoka mitungi ya oryex gas 115 yenye thamani kiasi cha Tsh. 5,175000/=.
Kwa shule za msingi 90 na shule za sekondari 19 zote kwa wilaya ya Chunya kwa ajili ya matumizi shuleni kwao na mitungi 6 waliweza kutoa kama zawadi kwa washindi wa michezo.
Sambamba na hilo Mhe. Masache kasaka ametoa Seti za jezi 10 kwa ajili ya michezo ambayo zilitumika kwa timu katika Wilaya zote 6 za mkoa wa Mbeya.
SAMIA NA MASACHE.
CHUNYA KAZI INAENDELEA




0 Comments