NAIBU WAZIRI MAHUNDI AKAGUA MINARA YA MAWASILIANO MKOA WA MOROGORO

Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi Leo Octoba 2,2024 amekagua minara miwili ya Kampuni ya Tigo iliyojengwa kwa ruzuku ya serikali kupitia mradi wa Tanzania ya kidigitali iliyopo katika Mkoa wa Morogoro. 


Aidha Mhe. Mahundi amewaomba wananchi kuwa walinzi wa kwanza wa hii miundo mbinu inayo jengwa Kwa gharama kubwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania pia amewahidi kuwa ifikapo mwakani mwezi Mei Minara yote 758 inayo endelea na ujenzi nchi nzima itakuwa imewaka ambapo mawasiliano yatakuwa yameimarika nchini hivyo kusaidia kochochea ukuaji uchumi wa kidigitali.





Post a Comment

0 Comments