Mbunge mteule wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ametekeleza ahadi yake ya kutoa shilingi milioni nne kwa ajili ya kutengeneza madisha kwa Msikiti Mkongwe uliopo Kata ya Nsalala Wilaya ya Mbeya.
Awali Mhandisi Maryprisca Mahundi aliahidi kutoa shilingi milioni mbili ambapo aliahidi kumshirikisha mgombea Ubunge Jimbo la Mbeya Vijijini Patali Shida Patali ambaye naye ametoa shilingi milioni mbili vivyo kufanya jumla ya shilingi milioni nne kukamilisha madirisha ya aluminium na vioo vyote.
Akipokea madirisha hayo Sheikh Rashid Msigala amewashuru Mhandisi Maryprisca Mahundi na Shida Patali Shida kufanikisha ujenzi wa madisha kwani imewaondolea kadhia ya mvua na upepo waliyoyokuwa wakiipata.
Mbali ya kukabidhi madirisha hayo Mhandisi Maryprisca Mahundi ametumia fursa hiyo kuwaomba waumini kudumisha amani na pia kuwahimiza kushiriki kupiga kura oktoba 29,2025.






0 Comments