Na Gordon Kalulunga Mwaipungu
NAWAPA Code za chekechea. Maendeleo yanaanzia kwa watu ndipo unaweza kusema vema kwamba tunaendelea. Huwezi kusomesha bila pesa.
Biblia inasema Pesa ni jawabu la mambo yote.
Tuwape watu wetu uwezo "Mfumo" wa kuwa na chochote mifukoni ndipo wataweza kujenga hata shule zao kwa michango yao.
Zaidi tutakuwa na Taifa la watu waishio kama walemavu waliolemazwa.
Tusiruhusu watu hawa kumtafuta anayewalemaza.
Kwenye ujasiriamali kumeanza kujaa. Kwenye Bodaboda kumeanza kujaa. Kwenye Bajaji kumeanza kujaa.
Je sisi viongozi tunajua viingilio vya kwenye vijiwe vya Bodaboda na Bajaji? Anayehusika aulize...
Hivi tumewahi kuwa na sensa ya watu walioishia kidato cha Nne na wapo mtaani au tunatazama tu wale ambao wameishia vyuo vikuu?
Ikitupendeza tujenge viwanda na kutoa elimu ya matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii badala ya kudhibiti. Uzuri ndugu yangu Mhe. Waziri wa vijana Joel Nanauka Joel Nanauka tupo naye kitambo kwenye mitandao ya kijamii naamini anafahamu ninachokisema.
Dunia inaambukizana tabia.
Tupunguze matumizi mabaya ya hasira.
Vijana wanataka kutengeneza kesho ya vizazi vyao kwa angalu kuangushiwa makombo.
Nampa Heko Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya ndugu Patrick Mwalunenge ameanza vema kuangushiana "Makombo" na wananchi wa mkoa wa Mbeya.
Mikopo ya asilimia 10 tutajadili wakati ujao.
Tusemezane maana kiti na meza ndiyo njia njema ya sote kutabasamu.

0 Comments