Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imeshiriki zoezi la upandaji Miti kwa lengo la kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa vitendo vya kulinda mazingira.
Akiongoza zoezi hilo Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi Januari 27, 2026 amesema lengo ni kuenzi maono ya Rais Samia la kutunza mazingira yanayotuzunguka.
Naibu Waziri Mahundi amempongeza Rais Dkt. Samia kwa uongozi wake kwa kuendelea kudhihirisha kiongozi maono, mbunifu wake na namna anavyojali maslahi ya Taifa
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amesema Wizara imeshirikiana na kundi la Wazee kuwakilisha Makundi Maalum yanayosimamiwa na Wizara katika zoezi hilo ambalo lina lengo kulinda na kutunza mazingira.
Nao baadhi ya Wazee kutoka Baraza la Wazee Mkoa wa Dodoma wamempongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Uongozi wake mahiri na thabiti katika kuliongoza taifa kwa misingi ya amani na utulivu.
Zoezi la upandaji Miti mbele ya Ofisi ya Waziri Mtumba Jijini Dodoma limehusisha Kundi la Wazee Mkoa wa Dodoma, Menejimenti na Watumishi wa Wizara hiyo.





0 Comments