POLISI KATA MBEYA WAJENGEWA UWEZO WA UTENDAJI KAZI KATIKA DHANA YA USHIRIKISHWAJI WA JAMII

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amewataka Wakaguzi na Askari Kata Mkoani humo kuendelea kutoa huduma bora kwa mteja.

 

Amezungumza hayo wakati akifungua Mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Wakaguzi na Askari Kata wa Mkoa wa Mbeya ili kuongeza tija na ushirikiano chanya na jamii hasa katika kubaini na kuzuia uhalifu.

 

Naye, Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Jamii kutoka Makao Makuu ya Polisi Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi Elisante Ulomi amesema kuwa lengo la Mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Askari hao hasa katika utoaji wa elimu, ushirikiano kati yao na jamii na katika suala zima la uanzishwaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi.

 

ACP Ulomi aliongeza kuwa ni matarajio ya Jeshi la Polisi mara baada ya mafunzo hayo, utoaji wa huduma bora kwa jamii utaimarishwa, ushirikiano kati ya Polisi na Jamii utaimarika na jamii itakuwa tayari kushirikiana katika kubaini na kutanzua uhalifu katika maeneo yao.

 

Kwa upande wao washiriki wa Mafunzo hayo, Polisi Kata ya Ilomba Jijini Mbeya Mkaguzi wa Polisi Athuman Kimeza na Polisi Kata ya Usongwe Sajenti Eliza Mwampaja wameeleza kuwa yatasaidia kuibadilisha jamii katika dhana ya kuzuia uhalifu, kuwajenga katika utoaji wa huduma bora kwa mteja ili kupunguza malalamiko na kuijenga jamii katika hali ya kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kurejesha Amani na Utulivu.

 

Mafunzo hayo yanatolewa katika Mikoa mbalimbali yakilenga kuwajengea uwezo Askari Kata na kurejesha Amani, Utulivu na Uzalendo miongoni mwa Wanajamii.

Post a Comment

0 Comments