Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi na Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mbeya ameshiriki ukaguzi wa ujenzi wa daraja la Lupatingatinga ambalo limekamilika na tayari limeanza kutumika.
Ujenzi wa daraja hilo ulitekelezwa na mkandarasi Summer Communication LTD kwa gharama ya shilingi Bilioni 5.6
Sambamba na hilo.
Mahundi amesema tuna kila sababu ya kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta Fedha za Ujenzi wa Daraja hilo ambalo lilikuwa adha kwa Wakazi wa Chunya hasa Msimu wa Mvua.
Aidha Mahundi amewasihi wakazi wa Chunya kuwa na subira kwenye Maeneo yote korofi na yanahitaji kuboreshwa serikali imeweka mpango na bajeti ili yaweze kujengwa hasa barabara hiyo ya Chunya - Lungwa itajengwa kwa kiwango cha Lami.




0 Comments