MJASIRIAMALI Frank Paskal mkazi wa Kata ya Nsalala Wilaya ya Mbeya ametoa wito kwa Watanzania kuhusika kulinda na kustawisha Amani.
Ameyasema hayo leo April 10,2026 Jijini Mbeya alipopata nafasi ya kutoa maoni yake juu ya umuhimu wa Amani na Utulivu Nchini.
Ndugu Frank amesema matukio ya Mwaka jana mwezi Oktoba hayapaswi kutokea tena katika Nchi yetu na ameshauri kwamba jamii inapokuwa na dukuduku na Serikali ni vema kuwasilisha hoja kupitia viongozi wa dini ama Viongozi wao wa Serikali za mitaa badala ya kujichukulia hatua za vurugu.
"Jukumu la kulinda Amani ni letu sote" amehitimisha Ndugu Frank Paskal.

0 Comments