WAUMINI WA KANISA LA ANGLICAN WAHIMIZWA KUKEMEA VITENDO VYA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI.


Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Anthony Mkwawa amewataka Waumini wa Kanisa la Anglican kupaza sauti kukemea vitendo vya uhalifu.

Hayo amezungumza Aprili 12, 2026 katika ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa la Anglican Dayosisi ya Nyanda za Juu kusini na kuhimiza viongozi wa dini na Waumini kutumia nafasi yao kupaza sauti kukemea vitendo visivyofaa katika jamii na ukiukwaji wa maadili.

Aidha, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mkwawa amewataka Waumini hao kutosita kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu na wahalifu kwa Jeshi la Polisi ili hatua stahiki zichukuliwe mapema ili kutokomeza uhalifu.

Naye, Polisi Kata ya Isanga Mkaguzi wa Polisi Lutygardis Felix amewataka Waumini hao kuimarisha malezi bora kwa watoto ili kuwajenga katika misingi mizuri na maadili mema na kujiepusha na vitendo vya uhalifu.

Post a Comment

0 Comments