MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBEYA WATEMBELEA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya leo wametembelea Baraza la Wawakilishi Zanzibar na kushiriki kufuatilia shughuli za Kikao cha 25 cha Mkutano wa 3 wa Baraza la 11 la Wawakilishi kilichofanyika katika Ukumbi wa Baraza uliopo Chukwani, Zanzibar.

Ziara hiyo imelenga kuwajengea uwezo madiwani hao kwa kuwapa fursa ya kujifunza namna chombo hicho cha kutunga sheria kinavyotekeleza majukumu yake ya uwakilishi, usimamizi wa shughuli za Serikali pamoja na utungaji wa sheria. Wakiwa ndani ya ukumbi wa Baraza, madiwani hao walipata nafasi ya kushuhudia mijadala mbalimbali iliyohusu makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Aidha uongozi wa Baraza la Wawakilishi ulieleza kuwa ziara za mafunzo kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa ni muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji na kubadilishana uzoefu unaosaidia kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kikao cha 25 cha Mkutano wa 3 wa Baraza la 11 la Wawakilishi ni sehemu ya mkutano wa bajeti unaojadili makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Ziara hiyo imehitimishwa kwa madiwani hao kutembelea maeneo mbalimbali ya Baraza la Wawakilishi na kupata maelezo kuhusu historia, majukumu na mchango wa taasisi hiyo katika kuimarisha utawala bora na maendeleo ya Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments