MAHUNDI AONGOZA MSAFARA MZITO WA TANZANIA MKUTANO WA COSP19 MAREKANI

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi, ameongoza msafara wa Tanzania kushiriki Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (COSP19) unaofanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Jijini New York, Marekani.

Mhe. Mahundi ameshiriki mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Profesa Palamagamba John Kabudi.

Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo unadhihirisha dhamira ya Serikali ya kuendelea kuimarisha utekelezaji wa haki, usawa, ujumuishwaji na ustawi wa watu wenye ulemavu nchini sambamba na kujifunza na kubadilishana uzoefu na mataifa mengine duniani.





Post a Comment

0 Comments