Mbunge wa Jimbo la Lupa-Chunya Mhe Masache N. Kasaka akiwa mgeni rasmi ameshiriki kumtambulisha mkandarasi aitwaye OBT COMPANY LTD katika mradi wa maji kata ya Lupa ambapo mradi utekelezaji wake utachukua mwaka mmoja na utagharimu kiasi cha Tsh.990,690,625/=.
Mhe Masache aliweza kuelezea mipango kazi na ahadi mbalimbali za miradi ikiwemo Miundombinu na Nishati,Elimu,Afya,Kilimo.
Sambamba na hilo Mhe Masache aliambatana na Mhe Kelvin Nshishi Diwani wa Lupa na Mwenyekiti wa halmashauri ya (W) Chunya, Mhe Rehema Kifwamba Diwani V/Maalumu,K/Siasa (W) wakiongozwa na Katibu wa CCM (W) Ndugu Jockery Selemani, Mkandarasi,Ofisi ya RUWASA (W) wakiongozwa na Engineer Sanga
Mhe Mbunge pia aliwahimiza wananchi kulinda amani na alimshukuru *Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan* Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kuendelea kutuletea fedha nyingi Wilayani Chunya kwenye Utekelezaji wa miradi mbalimbali.


0 Comments