Uzinduzi wa DIRA 2050 chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan unatajwa kuwa hatua ya kihistoria inayo kamilisha ndoto ya Mwalimu Julius Nyerere ya uhuru kamili wa Tanzania. DIRA hii siyo tu ramani; ni mkataba wa kazi unaoelekeza Taifa katika kilele cha uhuru kamili wa kiuchumi ifikapo 2050.
Mwalimu Nyerere alihakikisha uhuru wa Kisiasa mwaka 1961, huku akisisitiza kwamba uhuru wa kweli unahitaji kurudisha utu wa Mwafrika katika nyanja zote nne: kisiasa, kiuchumi, kiakili, na kiroho.
DIRA 2050 inaashiria mwanzo rasmi wa safari ya mwisho ya kulifikia lengo kuu la Kujitawala Kiuchumi.
Mafanikio ya DIRA 2050 yanategemea sana kizazi cha sasa cha vijana, ambao ndio injini ya uchumi wa baadaye. Dira hii inakuita wewe kijana, uachane na njia za mkato, uchochezi, na migogoro, na badala yake wajipange kufanya kazi kwa bidii na ubunifu huku wakiachana na ndoto ya kusubiri ajira za ofisini. DIRA 2050 inaweka msingi wa viwanda na teknolojia. Vijana wanatakiwa kutumia fursa hiyo kubuni miradi yako, kuanzisha biashara, na kuwa waajiri.
Aidha vijana wam,etakiwa kuthamini teknolojia kwa kuwekeza katika elimu ya ufundi na teknolojia , kujifunza ujuzi unaoendana na soko la kimataifa. Kazi yako yenye ubora ndiyo inaleta dola trilioni 1 iliyozungumzwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika yote hayo inawezekana ptu kwa vijana kujitambuua na kukataa uchochezi na kuchagua neema kwani mtaji mkuu wa maendeleo ni amani. Amani na Utulivu, inabaki kuwa sharti kuu. Matukio ya uchochezi na vurugu (kama yale ya Oktoba 29) hayana sura ya maisha yenye neema; yana sura ya hasara, uharibifu, na kurudi nyuma kwani wito wowote wa uvurugaji unadumaza lengo la nchi ya kipato cha kati cha juu kwa kufukuza mitaji inayohitajika kuunda ajira .
Kiukweli uhuru wa kiuchumi unarejesha utu. Uchochezi na vurugu vinaondoa heshima na utu wa Mwafrika ambao Nyerere aliupigania.
DIRA 2050 si ndoto ya mbali; ni mkataba na watoto wetu na wajukuu wetu. Ni wito wa kuacha kupiga magoti na kuanza kusimama imara kama Taifa huru kiuchumi.
"Tuheshimu imani iliyowekwa kwetu na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na tufanye kizazi chetu kuwa kizazi kitakachotoa Uhuru Kamili wa Kiuchumi kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tuanze leo! Fanya kazi kwa bidii, ulijenge taifa na ujiwezeshe wewe mwenyewe."

0 Comments