MKURUGENZI MTENDAJI AFUNGUA KIKAO CHA AWALI CHA BAJETI YA LISHE MBEYA DC .

NA MWANDISHI WETU, MBEYA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Bi. Erica E. Yegella, leo Disemba 29,2025 amefungua kikao cha awali cha bajeti ya lishe kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa halmashauri. 

Katika kikao hicho, ameeleza kuwa utekelezaji wa masuala ya lishe unaendelea kwa ratiba na kusisitiza umuhimu wa lishe bora katika kujenga jamii yenye afya na akili bora. Amehimiza halmashauri kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa lishe.

"Lishe inaenda kwa ratiba lakini pia tuwatangazie wananchi nini maana ya lishe bora na kwanzia sasa hivi nina elekeza tuko kwenye mpango na tuhakikishe kila maeneo yenye wananchi kwenye mbao za matangazo iwe zahanati iwe kwenye shule ziwekwe poster zinaozo onyesha chakula cha lishe bora "



Aidha, amesisitiza kuwa maafisa husika na idara zao wamepewa dhamana ya kuhakikisha bajeti ya lishe ya 2026/2027 inakuwa ya mfano, yenye uhalisia na inayotekelezeka.

Post a Comment

0 Comments