Sauti kutoka Nyikani
Na Tata Gordon Kalulunga Mwaipungu
NIHARAKISHE kusema kuwa Jiji la Mbeya halina sehemu ya wazi ya kukutana au twaweza ita Open Space.
1. Majiji karibu yote duniani sehemu ya kupumulia (mapafu ya mji) unaweza kuita Urban green area, or Public park au Green area.
Ni huduma muhimu kwa wananchi kufanya recreation. Kwamfano Dar. Es Salaam kuna Mnazi mmoja, Azania front na Dodoma kuna Nyerere Square na Open Spaces kibao.
2. Mbeya iko busy kujenga milimani na mabondeni makazi ya watu.
Mfano Juhudi, Kawetele, Mlima Loleza, Iwambi, Itende yote ni makazi.
Ukitaka kukutana na mtu au kujitafakarisha inakulazimu uende Bar au Hotelini Kwa wale wenye uwezo wa kifedha.
Huduma ya kucheza watoto hakuna sehemu ya kupumzika hakuna, open spaces zote zimeuzwa kwa mikataba isiyogusika na hakuna anayejali.
Maeneo yote yaliyokuwa wazi waitwao wataalam na wana siasa wamewapa wafanyabiashara.
Mbeya inajali zaidi pesa kuliko Afya.
Maeneo mawili ambayo yalikuwa ya kupumulia Jiji kwa Sasa yamewekwa majengo mazito ikiwemo eneo lililo Jirani na uwanja wa Sokoine na uwanja wa zamani wa Ndege ulio Jirani na kikosi cha Samora.
Kwa Sasa eneo Pekee ambalo ni tegemeo hata kwa matukio mengine ya Serikali na jamii ni eneo la Uhindini lilipokuwepo soko la Uhindini "Mwiboma".
Ikiwapendeza Madiwani na Wabunge eneo hilo linatakiwa libaki kama lilivyo kwa Sasa badala ya kulijenga maana ndiyo eneo Pekee la kupumulia Jiji la Mbeya kama Mapafu, vinginevyo Jiji la Mbeya litaendelea kupumulia Kichwani Kwa tamaa ya kiitwacho kuongeza mapato huku maafisa Mipango Miji, Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya wakiendelea kuja na kwenda kwao kwenye miji yenye Mapafu.
Ndiyo maana ninasema kuwa Mbeya haina Mapafu, inapumulia Kichwani.
Msiponielewa leo, mtanielewa kesho.
Karibuni sana Nyikani
0765615858

0 Comments