JAMII YATAKIWA KUKEMEA VITENDO VYA UKIUKWAJI WA MAADILI.

Wakazi wa maeneo ya Nsalaga Jijini Mbeya wamehimizwa kuzingatia kutoa malezi bora kwa watoto ili kuwajenga katika misingi mizuri na maadili mema.

Rai hiyo imetolewa na Polisi Kata ya Igawilo Mkaguzi wa Polisi Omari Issa Aprili 10, 2026 wakati akizungumza na wazazi na walezi wa Kata hiyo katika kikao kilichohusisha wakazi wa maeneo hayo.

Aidha, Mkaguzi wa Polisi Omari Issa aliwataka wazazi na walezi kukemea vitendo visivyofaa vya kimaadili vinavyofanywa na baadhi ya vijana katika jamii ikiwemo uhalifu na ukatili wa kijinsia kwani ni kinyume cha sheria za nchi.

Kwa upande wake, Polisi Kata ya Iduda Mkaguzi wa Polisi Paul Mruma ameitaka jamii kujiepusha na imani potofu za kishirikina kwani husababisha madhara katika jamii ikiwemo kulipiza visasi na jinai.

Mruma ameitaka jamii kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama kupitia vikundi vya ulinzi shirikishi ambavyo vitafanya kazi ya doria za usiku na mchana ili kulinda usalama wa raia na mali zao.

Post a Comment

0 Comments