MARAIS WASTAAFU WA LIBERIA NA ETHIOPIA WAHITIMISHA ZIARA NCHINI

Rais Mstaafu wa Liberia, Mhe. Ellen Sirleaf na Rais Mstaafu wa Ethiopia, Mhe. Sahle-Work Zewde wamemaliza ziara ya kikazi nchini Tanzania na kurejea katika nchi zao.

Waheshimiwa Marais Wastaafu wamefanya ziara nchini kama wawakilishi wa Mtandao wa Wanawake Viongozi Barani Afrika (African Women Leaders Network -AWLN), wakiongozwa na Mhe. Sirleaf, ambaye ni Mlezi wa mtandao huo.

Wakiwa nchini, Mhe. Sirleaf na Mhe. Zewde wamepata nafasi ya kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nie na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. James Millya (Mb.) akiambatana na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb.) wameshiriki kuwaaga viongozi hao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Post a Comment

0 Comments