BAADA YA KIPIGO: KOCHA MADRID AWAANGUSHIA MZIGO WACHEZAJI

KOCHA wa Real Madrid, Julen Lopetegui amewashushia lawama wachezaji wake kuwa hawakucheza vizuri katika mchezo waliokubali kichapo cha mabao 3-0 toka kwa Sevilla.

"Maelezo ni kwamba tuliuanza mchezo vibaya na tumecheza vibaya. Sevilla walianza vema mchezo wakifunguka na kupata mabao mawili ya mapema, sisi hatukuwa vizuri. .

"Kipindi cha pili tulianza vizuri tukatengeneza nafasi nyingi ambazo hazikuzaa mmatunda, lakini hakuna namna, tunapaswa kukubali matokeo na kuwapongeza Sevilla."

Post a Comment

0 Comments