Cristiano Ronaldo ,34,  Mpaka sasa amefanikiwa kufunga magoli 30 katika michezo 48 akiwa ametinga uzi wa juventus toka ajiunge nao Msimu uliopita.

Ronaldo ameweka rekodi ya kuwa mpiga Faulo ( Free - kick ) Mbovu namba mbili kuwahi kutokea katika ligi kuu  italia maarufu kama Serie A.

Ronaldo amepiga mikwaju 18 kwa michezo ya Seria A Tangu ajiunge na  juventus. Lakini ukijumlisha na zile Free- kick sita za Champions league zinakuwa 24.

Katika hizo free-kick 24 , 15 zilibamiza ukuta , 7 ziliokolewa na walinda milango na 2 alikosa shabaha kabisa ( alipiga minazi ).

Anaye shikilia nafasi ya kwanza kwa upigaji mbovu wa free-kick ni  anaitwa Camillo ciano alipiga free-kick 21 mfululizo pasipo kufunga goli kwa kipindi chote alichocheza italia akiwa na Napoli.

NB: Cristiano ronaldo akiwa Real madrid aliPiga free-kick 313 na kufanikiwa kufunga 20 tu. ⚫️

[ source The sun ]