Na Gordon Kalulunga
AINA ya siasa anayoifanya Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Ndugu Ndele Mwaselela ni ngumu sana.
Akiamua kugombea popote basi watu wajiandae Kisaikolojia.
Kwenye U-NEC wakubwa wengi hawakuwa naye wakiwemo wenye pesa lakini akashinda.
Lakini tumeona ziara yake aliyoifanya Mbeya Vijijini hivi karibuni kwa ajili ya kuimarisha chama chake yaani CCM.
Ziara yake imezaa matunda makubwa ikiwemo baadhi ya Wana siasa kuwapa vibarua vijana kwa ajili ya kuwasaidia katika mambo kadhaa ya kiuenezi na kupata chochote.
Ndugu Ndele Mwaselela ni kama Mkaa safi.
Unapomsifia mwenye mbio jua kuna mtu mwenye jitihada za kumfukuza.
Ndiyo maana ninasema kuwa ashukuriwe M-NEC Ndele Mwaselela kwa kuleta ajira/vibarua za dharula Mbeya Vijijini.

0 Comments