TUSIMUONEE ABDUL HAFIDH AMEIR KWA KUMUNGANISHA NA RAIS SAMIA



Na Gordon Kalulunga 

NIMESOMA katika kurasa za Intagram na X Habari/hadithi za tuhuma kadhaa zikimtaja Rais Samia Suluhu Hassan na Abdul Hafidh Ameir ambaye ni Mwanaye.

Sioni kama ni haki kumuunganisha kijana huyu na nafasi ya Rais Samia Suluhu Hassan katika tuhuma mbalimbali.

Tuanzie hapa👇🏽

Ijulikane kwamba mtu akiwa Rais au kiongozi wa ngazi yeyote au mgombea basi ajue kuwa nusu ya faragha yake imepunguzwa.

Uongozi unapunguza faragha yako.

Ninachotaka kusema ni kwamba anaweza kusemwa Rais hata kwa kusingiziwa lakini asiingizwe mtu asiye kiongozi kisa tu ni mtoto wake.

Haya mambo yaliwahi kutokea huko nyuma kuhusu Ridhiwan Jakaya Kikwete akihusishwa na mambo ya Baba yake Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa madarakani.

Kama lipo jambo la Abdul pekee lisemwe kwa upekee wake lakini sioni kama ni vema kumuambatanisha na nafasi ya Rais ambaye ni mama yake ingawa sisemi kuwa naunga mkono kusemwa Rais Samia Suluhu Hassan katika yasiyo haki.

Ndugu Salim Alkhasas amefafanua vema katika ukurasa wake kuhusu biashara za wazi kabisa za Ndugu Abdul pale Kariakoo huku andiko lake likichagizwa na Ndugu Enock Kiswaga kuwa wengi wanaomzushia mambo Abdul na kumtukana hawamjui.

Ndiyo maana ninasema kuwa Abdul Hafidh Ameir asiunganishwe na Rais Samia Suluhu Hassan.

0765615858

Post a Comment

0 Comments