Sauti kutoka Nyikani
Na Gordon Kalulunga
MHESHIMIWA Mhandisi Maryprisca Mahundi ni Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya.
Pia ni Naibu Waziri wa Habari na Teknolojia ya habari nchini.
Ni Mbunge wa umri wa kati ambaye hata tabasamu lake linaonesha kuwa kweli ni Mbunge wa watu.
Mbunge huyu tangu apate nafasi hiyo amepandisha thamani ya nafasi hiyo tofauti na awali namna ambavyo watu walivyokuwa wanautazama.
Hapa twende taratibu angalau kwa ufupi
Awali watu wengi walidhani nafasi hiyo ni kwa ajili ya viongozi wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM pekee (UWT), lakini yeye ameupandisha hadhi Ubunge huo kwa kuhudumia wanawake wote bila kujali itikadi za siasa au vyeo.
Anafanya kazi za kibunge na kukijenga chama chake ndani ya chama na nje ya chama, hali ambayo chama kinazidi kunukia katika mioyo ya watu.
1. Hivi karibuni alipiga mbiu ya wanawake wote wanaojihusisha na shughuli za mama Lishe na kuwagawia mitungi ya gesi safi za kupikia ilikuwa ni hamasa ya wanawake kupunguza kutumia Mkaa na Kuni kupikia ili kuungana na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwezesha jamii kutumia nishati safi ya kupikia na kutunza Mazingira.
2. Mkono wake siyo mzito....
3. Hivi karibuni ameonekana akikichangia chama chake kiasi cha Shilingi Milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa CCM Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
Pia ameonekana akitoa mchango wake wa simu za viganjani kwa viongozi wa UWT Wilayani Chunya kuelekea uchaguzi Mkuu wa Serikali za mitaa.
Wahenga wanasema uzuri wa mti siyo wingi wa majani yake bali ni matunda uzaayo.
Maryprisca ni kimbilio la watu wengi kutokana na matunza yake na roho yake ya utoaji na hajawahi kukivaa cheo, bali yeye kabaki kuwa Maryprisca.
Ndiyo maana ninasema kuwa Maryprisca Mahundi anaupa thamani halisi Ubunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya.
Naomba kutoa hoja.
0765615858


0 Comments