Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Songwe wakiongozwa na Mwenyekiti wao Emilia Mwakyoma, wameanza ziara ya Kata kwa Kata ndani ya Wilaya ya Songwe yenye lengo la kuhamasisha Wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Wajumbe hao wanahamasisha wanawake wenye sifa za kugombea kujitokeza katika kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi tarajali wa Serikali za mitaa mwaka huu 2024.
Sanjali na hayo ajenda nyingine ni kukemea vitendo vya kikatili ikiwemo mimba za utotoni ambazo imekuwa ni tatizo kubwa katika Mkoa huo wa Songwe pamoja na kuhimiza ustawi wa Umoja huo na CCM kwa Ujumla.
0 Comments