Na Gordon Kalulunga
NAIBU waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi (Pichani), ni kiongozi aliyezawadiwa dhabihu ya utoaji.
Kiongozi huyu mbali na dhabihu ya utoaji, pia ni kiongozi ambaye anatambua kuwa uzoefu pekee katika uongozi haumfanyi mtu kuwa kiongozi mzuri bali kujifunza kwa wadogo na wakubwa ndiko kunamfanya mtu kuwa na ushupavu wa uongozi.
Septemba 20,2024 akiwa mgeni rasmi wa Mahafali ya Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Ilemi iliyopo Kata ya Iganzo jijini Mbeya, aliwasihi Wazazi kote nchini kuwa karibu na watoto wao wa kike na Kiume na kuwasikiliza na kuwafundisha namna ya kukabiliana na matendo ya ulawiti na ubakaji.
Aliyasema hayo baada ya kusikiliza Ngonjera ya watoto wa Kiume wa Shule hiyo ambayo iliwatoa machozi watu kadhaa waliohudhuria sherehe ile.
Pia alitoa rai kwa wavulana wale kutoyaweka moyoni na akilini yale waliyoyaghani ili kutotengeneza athari za Saikolojia kwao.
Akiwa shuleni hapo, Mheshimiwa Maryprisca Mahundi alitoa Kompyuta 2 na Magodoro Matatu kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum pia ameahidi kutafuta Viti mwendo Saba, kwa ajili ya wahitaji wa shule hiyo.
Katika utoaji huo, pia yeye atazidi kupata tabasamu mara dufu kutoka kwa Mungu.
Ndiyo maana ninasema kuwa, Maryprisca Mahundi ni Mbunge anayefahamu kuwa alizaliwa kwa ajili ya kuwapa tabasamu wengine.
0765615858



0 Comments