PARADISE MISSION WAZAZI NYAMA CHOMA FESTIVAL, NDELE MWASELELA ANATUFUNDISHA KUWA NA SHUKRANI

 


Na Gordon Kalulunga 

TAMASHA la uchomaji na ulaji wa nyama lililoandaliwa na Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Paradise Mission Pre and Primary School ya Mbalizi nje kidogo ya Jiji la Mbeya Ndugu Ndele Mwaselela, limefanyika leo Oktoba 26,2024.

Tamasha hilo lililojulikana kwa jina la Paradise Mission Wazazi Nyama choma Festival, lilikuwa mahususi kwa ajili ya kuwashukuru Wazazi wote ambao wanasomesha watoto wao katika shule hiyo ya Paradise Mission na kumshukuru Mungu kwa wanafunzi wa Darasa la Saba na Darasa la Nne kumaliza salama mitihani yao.

Pamoja na uwepo wa nyama choma ya Ng'ombe Watatu na Mbuzi Nne, wanafunzi wa Shule hiyo wamepata wasaa wa kuburudika na michezo ya kuogelea, kuserereka na kuendesha Baiskeri zenye Mwana Sesere (Midori).

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Rozarina Mtumbuka amewaambia Wazazi waliofika shuleni hapo kuwa lengo la tamasha hilo ni kuwashukuru Wazazi hao pamoja na kumshukuru Mungu kwa mafanikio ya shule hiyo katika taaluma na maadili.

Mmoja wa Wazazi aliyejitambulisha kwa jina la Christina, amesema wanaushukuru uongozi wa Shule ya Paradise chini ya Mkurugenzi wake Ndele Mwaselela kwa kuona umuhimu wa kumshukuru Mungu pamoja na Wazazi hao katika suala hilo la shukrani kwa wanafunzi wa Darasa la Nne na darasa la Saba kumaliza salama mitihani yao.

Ni shule chache ambazo zina utaratibu wa namna hii, ndiyo maana ninasema kuwa Ndele Mwaselela anatufundisha kuwa watu wa shukrani.

Post a Comment

0 Comments