MHANDISI MAHUNDI AMPOKEA MWENZA WA RAIS WA MALAWI



Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Kulia) Leo Tarehe 28 Oktoba 2024, amempokea mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Monica Chakwera ambaye atakuwepo Nchini kwanzia Tarehe 28 Oktoba mpaka Novemba 1, Mwaka huu wa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa 11 wa Merrick Foundation Africa Asia Luminary, utakao fanyika kuanzia Tarehe 29 hadi 30 Oktoba, 2024 katika hotel ya Johari Rotana iliyopo Jijini Dar es salaam.

Aidha , Mkutano huo unatarajiwa kuwakutanisha wenza wa Marais 24 kutoka Nchi mbalimbali Barani Africa na wengine takriban 500 kutoka nchi mbalimbali Duniani, na Mgeni rasimi katika Mkutano uwo anatarajiwa kuwa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.




Post a Comment

0 Comments